TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

ALI SULEIMAN

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

 

Taasisi ya Karume inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:

1. MUANGALIZI WA OFISI DARAJA LA TATU NAFASI MOJA (1)

             Sifa za kuajiriwa

Muombaji awe mwenye diploma ya utawala/Uongozi au inayolingana na hiyo kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na GPA isiyopunguwa 3.5

                   KAZI

 • Kuandaa mipango ya matumizi ya Ofisi.
 • Kuhakikisha vifaa vya ofisi vinaingizwa kwenye leja.
 • Kusimamia vifaa vya ofisi na kuhakikisha vinatumika ipasavyo.
 • Kuhakikisha vifaa vya ofisi vinakuwa katika hali nzuri ya matumizi.
 • Kuhakikisha kuwa ofisi zote zina wafanyakazi wa kutosha kwa shughuli za kila siku.
 • Kuandaa mipango ya usafiri kwa watumishi wanaosafiri kikazi.
 • Kuandika hati za mahitaji (LPO) na kuhakikisha ankara zote zinapelekwa haraka sehemu ya hesabu kwa malipo.
 • Kufanya kazi nyengine za halali atazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

 

 

2. UDEREVA DARAJA LA III NAFASI MOJA (1)

 

Sifa za kuajiriwa:

 • Muombaji awe mwenye cheti cha elimu ya lazima, na cheti cha udereva na kupata leseni daraja (D) ya gari na kuendelea kutoka katika Taasisi inayotoa leseni na kutambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kazi

 • Kuchunguza na kuikagua gari atayopangiwa kazi kabla ya kuanza kutumika kila siku ya kazi.
 • Kuhakikisha kuwa gari inakuwa safi wakati wote.
 • Kufanya matengenezo madogo madogo, kama kuweka vilainishaji, kubadilisha mpira, kuweka maji n.k
 • Kuhakikisha kuwa gari haina hitilafu yeyote wakati akiwa yumo kwenye safari ya kazi.
 • Kujaza “Log Book” kabla ya kufanya safari aliyopangiwa, kwa kazi za Taasisi ya Karume.
 • Kuegesha gari wakati linapomaliza shughuli zake za siku ndani ya eneo la Taasisi ya Karume na kuikabidhi kwa Walinzi wa zamu, na kama kutakuwa na khitilafu ya wazi kuwapa taarifa ya khitilafu hiyo.
 • Kutoa taarifa kwa Mkuu wake wa kazi juu ya haja ya kufanyiwa matengenezo gari baada ya kujulikana tatizo la gari ambayo imepata maharibiko
 • Kuwa tayari kufanya safari yeyote ya kazi na kwa wakati ataopangiwa na Mkuu wake.
 • Kuweka na kufuata kumbukumbu ya wakati wa gari kupelekwa karakana kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa kawaida (regular service).

 

NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI.

Muombaji anatakiwa andike barua ya maombi kwa mkono na kuiambatanisha na mambo yafuatayo:

 1. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.
 2. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
 3. Picha moja ya muombaji (passport size).
 4. Nambari ya simu.
 5. Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi.
 6. Maelezo binafsi (C.V) pamoja na kipengele cha wadhamini wasipungua watatu.

 

              MAMBO YA KUZINGATIA KWA MUOMBAJI.

 1.  Muombaji atakaewasilisha ‘’Statement of result’’ au ‘’Progressive report’’ maombi yake hayatazingatiwa.
 2.  Muombaji anatakiwa ainishe nafasi moja anayoiomba kati ya kazi zilizotajwa hapo juu. vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
 3.  Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni siku ya Jumatatu  ya tarehe 10/06/2019
 4. Mawasilino yatafanywa kwa wale tu watakaopita katika mchujo wa awali yaani (short listed).
 5. Maombi yawasilishwe Taasisi ya Karume  kwa anuani ifuatayo:

MKURUGENZI,

TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA,

S.L.P. 467,

ZANZIBAR.

Tangazo hili pia linapatikana pia katika tovuti ya Taasisi ya Karume www.kist.ac.tz na katika    ubao wa Matangazo uliopo KIST.

 

            Ahsanteni.

BY

UTAWALA

KIST

30/05/2016

 

Related Posts you may like